16/05/2021
© Millard Ayo

MAELEKEZO MAKALI YA WAZIRI JAFO KWA WANAOJENGA HOTEL KWENYE FUKWE ZA ZIWA NA BAHARI

Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa rais Muungano na Mazingira Selemani jafo ameagiza kwa ujenzi na uwekezaji unaofanywa karibu na fukwe za Bahari na Maziwa kote nchini kupata kwanza vyeti vya mazingira ili kuepusha uharibifu wa miundombinu unaondelea kutokea kwa sasa.

Selema Jafo ametoa maagizo hayo katika ziara yake aliyofanya katika Manispaa ya Kigoma ujiji mkoani Kigoma baada ya kutembelea maeneo kadhaa ya uwekezaji wa hoteli yaliyoathirika kutokana na kujaa kwa ziwa Tanganyika.

Mabadiliko ya tabia ya nchi na Mvua zinazoendelea kunyesha zinatajwa kuwa sababu zinazochangia ongezeko maji katika Ziwa Tanganyika na kuweza kufikia takribani mita nne kutoka usawa wa maji na kupelekea uharibifu wa miundoi mbinu kadhaa iliyojengwa  kando kando mwa ziwa Tanganyika katika manispaa ya Kigoma Ujiji.
x

Login to Chop


Sign in with Google Continue with Google
Sign in with Linkedin Continue with Linkedin

OR

Login using your Gapeli account

OR
Create a Gapeli account